Friday, February 27, 2015

Tunaelimishaje watoto wetu na wa jirani zetu? NO. 5b




      “Mazingira magumu” neno mazingira pia lina maelezo mengine yakufanana nalo ambayo ni mandhari, hali, zunguka, zingira, zingia, na zinga. Hivyo “magumu” ni kivumishi cha kuoneshea ni kwa namna gani hayo mazingira yalivyo. Kama ukisema ni hali ngumu pia inaendana na dhana nzima ya mazingira magumu katika hoja yangu ya msingi.

    Mazingira magumu huwa yanatofautiana kati ya kaya moja na kaya nyingine, watoto wanaoishi katika mazingira magumu wana tofautiana pia katika hali wanazopitia katika maisha yao. Kupata wazazi au walezi wasiothamini elimu wala kuona umuhimu wa watoto kupata elimu, ni mazingira magumu ya awali ambayo kwa namna ya kipekee hayawezi kumpa mtoto hamasa ya kupenda kusoma.

   Katika makala zilizotangulia niligusia suala zima la upendo wa wazazi kwa mtoto, mama na baba na ndugu wa karibu wa familia wana nafasi kubwa katika kumjengea mtoto mazingira mepesi kuelekea mafanikio yake ya kielimu. Tukumbuke watoto wanazaliwa wakiwa na uwezo wa kiakili na ufahamu wa kiasi tayari kwa kuanza kujifunza mambo mengine kadiri ya mazingira atakayokutana nayo.

    Agizo kuu la awali la Mungu kwa Adamu na Eva ilikuwa ni la kuzaa na kuongezeka ili wapate kuijaza dunia, hivyo uwepo wetu hapa duniani wa mtu mke na mtu mume ni katika kutimiliza upendo huo mkuu toka kwa Mungu. “Kuzaa si kazi, kazi kulea mwana” ni msemo wa kawaida sana kuusikia linapokuja suala la mjadala kuhusu watoto na malezi yao. Tatizo kubwa lililopo ni kwenye tafsiri ya maneno yanayotumika katika suala zima la mawasiliano, ukichukulia kauli hiyo ya kazi kulea mwana kila mmoja anaweza kuwa na fikra tofauti lakini mimi naweza kukwambia kulea ililenga katika dhana ya kumwelimisha mtoto.

       Mungu ndiye chanzo cha maarifa yote, Mungu ni hekima ipitayo hekima zote katika kuona ukweli huo katika kitabu kitakatifu cha Biblia katika kitabu cha Mithali, “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa” ni kauli aliyotoa Mwenyezi Mungu ikionesha umuhimu wa maarifa ili watu wa Mungu wasiangamie. Katika hili ndipo wazo la Baba na Mama ni miungu wa dunia usije kulisahau na kulipuuzia. Kwani Baba na Mama ni wa kwanza katika kuhakikisha mtoto wao anapata maarifa stahiki, nadhani ndugu msomaji umeanza kupata picha sasa ya namna ya kutenda kadiri inavyopasa.

      Mazingira magumu yanaweza kufanana na haya yafuatayo, mtoto kutozungukwa na watu wenye mwamko wa kielimu, ikiwemo mtoto kuzaliwa katika ukoo usio na mwamko wa kielimu, mtoto kuzaliwa katika familia hohehahe yenye kipato duni kisichotosheleza hata kupata mlo wa siku moja. Mtoto kulelewa na mzazi mmoja iwe baba au mama, mtoto kulelewa na bibi na babu, mtoto kulelewa na ndugu na jamaa, mtoto kuzaliwa katika eneo lenye utamaduni usiojali elimu, mtoto kuzaliwa katika eneo lenye mtazamo hasi kuhusu masuala ya kielimu, mtoto kuzaliwa katika wakati ambao Taifa halina mwelekeo mzuri wa kielimu wala mipango ya kujikwamua katika kuwekeza kwenye elimu ya watoto. Hiyo ni mifano ya baadhi tu ya mazingira magumu ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya kielimu ya mtoto.

Kila aina ya mfano wa mazingira magumu unaweza kupata maelezo mengi tofauti kwa kuwa namna ya kukabiliana na mazingira hayo pia inatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Jambo la msingi kabisa ni mwamko wa kielimu wa jamii husika ambayo mtoto huyo atakuwa amezaliwa. Jamii hiyo inachukuliaje suala zima la elimu? Kwa namna ya kipekee katika hoja hii nitapenda kuelezea pia na uzoefu wangu katika maisha haya tunayoweza kuita ya mazingira magumu.

Kijana “Kung’alo” jina la kubuni, ni mzaliwa wa kaya duni kama zilivyo kaya nyingi za hapa Tanzania amepitia katika mazingira mengi magumu ya kimaisha. Lakini kwa upendo na msaada mkubwa wa Mungu ameweza kujifunza masuala mbalimbali ya kijamii.  Katika familia yao walizaliwa watoto takriban nane (8) katika jiji la Dar es salaam, jiji lililojaa kila aina ya pilika tangu enzi za utawala wa awamu ya kwanza baada ya kupata uhuru.

Wazazi wao hawakuwa waajiriwa, ni baba ndio alikuwa chanzo cha kipato cha familia kwa hivyo kulikuwa na changamoto mbalimbali katika maisha ya familia hiyo. Kung’alo akingali mdogo yeye na ndugu zake baba yao alianza kuingia katika ulevi wa kupindukia ambao kwa namna kubwa ulisababisha kuyumba kwa familia kwani kipato kidogo alichokuwa akipata baba huyo, pia kilifanyiwa matumizi mengine ya anasa za dunia.

Wakati wa kuanza kujiunga na shule ulipowadia kadiri ya umri wa Kung’alo ambaye ndie alikuwa wa kwanza kuzaliwa alienda kuanza darasa la kwanza. Wakati huo umri wa kuanza darasa la kwanza ilikuwa ni miaka 9 na 10, akawa na maendeleo mazuri darasani alipofika darasa la tatu na mdogo wake Kung’alo alianzishwa darasa la kwanza na yeye. Familia hiyo ilikuwa na utaratibu huo wa kuwapishanisha madarasa mawili watoto wao ikishabihiana na tofauti yao ya umri wa kuzaliwa.

Watoto wa kaya hiyo walikuwa na uwezo mkubwa wa kiakili kwani walikuwa na maendeleo mazuri katika masomo yao tangu ngazi ya awali. Maisha yao yakazidi kuwa magumu kwa vile sasa mahitaji yakawa mengi zaidi yakiongezeka na gharama za shule, kwani ili watoto waendelee vema na masomo kuna wakati walilazimika kwenda twisheni na kufanya mitihani mbalimbali ya majaribio. Kwa hakika pongezi kubwa inastahili kwenda kwa mama yao mzazi bwana Kung’alo na wadogo zake. Mama huyo alihakikisha watoto zake wanapata elimu, alikuwa na juhudi kubwa ya kufuatilia mwenendo wa watoto zake.

Mama huyo alikuwa na utaratibu wa kuwatambua walimu wa darasa kwa kila mtoto wake, hivyo kwa utaratibu huo aliweza kufahamiana na walimu wengi sana shuleni walipokuwa wanasoma watoto zake. Jambo la kipekee ni kwamba mama huyo aliamua watoto zake wote wasome katika shule hiyo hiyo, nadhani akiwa na lengo madhubuti la kuwafuatilia kwa ukaribu zaidi kuliko wangekuwa kila mmoja anasoma katika shule tofauti. Alishiriki kila kikao cha wazazi wa wanafunzi pale walipokuwa wanahitajika kufika shuleni kusikiliza mipango ya shule hiyo.

Wakati wote huo baba yao kina Kung’alo yeye alikuwa akiendelea na mabadiliko yake ya maisha ya anasa ilhali kipato chake pia hakikuwa cha kuridhisha. Kadiri hali ilivyozidi kuwa ngumu, ndipo mama yao kina Kung’alo akaanza kujishughulisha na biashara mbalimbali ndogondogo katika jitihada za kupunguza ugumu wa maisha na kupata pesa za kusaidia maendeleo ya watoto shuleni. Kung’alo na wadogo zake nao hawakuwa nyuma wakisaidiana na mama yao katika kutafuta ridhki kwa ajili ya mahitaji ya familia. Mungu akaendelea kuwajalia vijana hao, wakaendelea vema na masomo yao bila ya kukatishwa tamaa na mazingira waliyokuwa nayo.

Kung’alo alifanikiwa kufaulu vema katika mitihani yake ya darasa la saba na kuchaguliwa kwenda sekondari, kwa wakati huo jambo kama hilo lilikuwa ni la kipekee waliokuwa wanafaulu na kuchaguliwa walistahili kwelikweli kwa vile walikuwa na akili na vipaji sana. Na kwa hali ya ufinyu wa shule kwa wakati ule idadi ya waliochaguliwa ilikuwa ni ndogo sana, lakini haikuwa kwa kijana huyo Kung’alo.
Ikawa hivyo hivyo na kwa wadogo zake Kung’alo walifanikiwa kupata nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari, ikawa ni furaha kubwa kwa mama yao hasa juhudi kubwa aliyoifanya kuhakikisha watoto zake wanasoma. Baba yao alikuwa akijivunia vipaji vya watoto hao kwa kujinadi kuwa amefanikiwa kuwasomesha watoto zake, kinyume na hali ilivyokuwa kwani ni mama yao ndio alikuwa shujaa wa elimu yao. Hata walipokuwa wakilala bila ya kula mlo wa usiku lakini bado vijana hao walilazimika kuamka mapema na kuwahi namba shuleni.

Ni kama walitambua kwamba elimu ndio itakuwa mkombozi wa familia yao kwa siku zijazo, walikuwa na juhudi kubwa ya kusoma wakichagizwa na uwezo mkubwa wa kiakili waliozaliwa nao. Mazingira mbalimbali ya kukatisha tamaa walikumbana nayo ikiwemo ya kukosa chakula iwe asubuhi, mchana na usiku lakini linapokuja suala la shule walikuwa mstari wa mbele. Walikosa pesa ya kulipia twisheni, walikosa ada, upatikanaji wa ada ulikuwa ni wa kukatisha tamaa walipokuwa katika shule za sekondari lakini waliendelea kupenda elimu.

Kuzaliwa katika mazingira magumu sio kigezo pekee cha mtoto kushindwa kufanya vema katika masomo yake, lazima viwepo vichocheo vingine vya kufanya ugumu huo ukawa kikwazo. Katika maelezo yote ya makali hii ukiangalia unagundua kwamba huwezi kufanya jambo lolote pasipo kuwa na sehemu ya kusimamia. Hata wajenzi wa nyumba huwa wanaanza na msingi katika kusimamisha jengo lao, ndivyo ilivyo kwa mtoto anayezaliwa katika mazingira magumu ili aweze kuendelea vema ni budi apate sehemu ya kusimamia.

Kuwepo na mtu wa kumsimamia na kumwongoza, ni kweli wapo wanaozaliwa na kipaji cha kujipa motisha na hamasa wao wenyewe. Watu wa aina hiyo wanao uwezo wa kusaka msaada popote pale wanapoona panafaa, ila kwa kiasi kikubwa tunao watoto ambao hawana vipaji vya namna hiyo. Na hakuna wataalamu wa kuwezesha utambuzi wa jambo hilo, walimu wetu hawaandaliwi kufanya jambo hilo kwa watoto wala wazazi wao.

Lakini ukweli wa jambo hili ni kwamba, inawezekana kabisa kumtambua mtoto amezaliwa kuwa nani katika maisha yake yajayo, zipo elimu nyingi za kuwezesha utambuzi wa jambo hilo, kuna elimu za saikolojia, filosofia, sosholojia, elimu ya unajimu na malezi mbalimbali. Wazazi ndio wangekuwa wa kwanza sasa kupewa maarifa hayo ili wajue namna ipasayo kulea watoto wao, elimu hiyo wazazi wanaweza kuipata kupitia viongozi wao wa dini, kupitia waelimishaji rika, na wafanyao kazi za kutoa ushauri wa malezi.




Nb: Mada hii itakuwa na mwendelezo wake kwa kuendelea kujadili suala la elimu kwa mapana yake, ili wazazi na wadau wa elimu kupata nuru ya kufanya maamuzi sahihi.

By Mkoba Andrian.

Friday, February 20, 2015

Tunaelimishaje watoto wetu na wa jirani zetu? NO. 5





“Kama elimu ni ghali, jaribu ujinga” sio msemo mgeni huu masikioni mwako, hilo naamini ni jambo lililo wazi kabisa kwetu sote ya kwamba elimu ni ghali hasa katika maisha ya sasa. Elimu imekuwa ghali sana kutokana na mabadiliko mbalimbali ya kimaisha duniani kote na hapa Tanzania pia. Kipindi cha ukoloni na miaka ya mwanzo ya uhuru elimu ilitolewa bure kwa wananchi kwa kuwa idadi kubwa ya watu ilikuwa haina elimu ya kimagharibi.

Na pia kulikuwa na idadi ndogo ya watu hivyo serikali iliweza kumudu kugharamia maisha ya watu wake katika upatikanaji wa elimu na masuala mengine ya kijamii. Kumbuka katika makala ya awali nilizungumzia kuhusu aina kuu tatu za elimu, linapokuja suala la elimu rasmi basi moja kwa moja tunazungumzia elimu yenye asili ya kimagharibi. Hivyo kwa upatikanaji wa aina hiyo ya elimu tunaingia rasmi katika mfumo wa maisha ya kimagharibi, kwa hiyo hakuna namna ya kukwepa moja kwa moja gharama ya elimu kwa kuwa upatikanaji wa elimu hiyo ni wa gharama.

Kwa kuzingatia hilo la gharama ya upatikanaji wa elimu rasmi, ndipo tuendelee kujadiliana hoja yetu ya msingi kuhusu namna ya kuelimisha watoto wetu na wa jirani zetu. Katika hili nianze kusema wazi kabisa watoto wengi huwa wanazaliwa wakiwa safi kabisa katika afya zao za mwili, roho na akili. Ingawa pia wapo kwa idadi ndogo wale wanaozaliwa wakiwa na hitilafu. Kila mtoto anapozaliwa huwa amezaliwa kutimiza lengo maalumu nikiwa na maana ya mtoto wako ndugu msomaji na mtoto wa jirani yako pia. Hivyo kwa pamoja watoto hao ndio wanaweza kuendeleza gurudumu la maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla wake.

Akili ya mtoto anapozaliwa haina uhusiano wowote na uwezo wa kiuchumi wa wazazi waliomzaa. Ila kuna uwezekano mkubwa wa mtoto huyo kuwa na vinasaba vya akili inayofanana na hao wazazi wake waliomzaa. Kumbuka ule msemo maarufu wa “Mtoto wa nyoka ni nyoka” nao unaweza kuleta maana katika maelezo yangu hapa kuhusu akili ya mtoto kurandana na ile ya wazazi wake. Kama mwanazuoni wa kijapani Okumura (2010) alivyoelezea katika ripoti yake ya utafiti juu ya ushawishi wa wazazi katika tabia za watoto wao. 

Ni wazi sasa unaweza kujiuliza maswali kadhaa ikiwa suala zima la elimu linakuwa hivyo je watu walio maskini wa kipato na watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanawezaje sasa kupata tunu ya elimu kama ilivyo kwa watoto wanaozaliwa katika mazingira mazuri ya kipato? Pamoja na maswali mengine yafuatayo;

·         Jukumu la elimu ni la nani?
·         Watoto wanaoishi katika mazingira magumu ni jukumu la nani kuwapatia elimu?
·         Jamii inawapokeaje watoto wanaoishi katika mazingira magumu?
·         Mazingira magumu ni yepi kwa watoto?
·         Nani anasababisha mazingira magumu kwa watoto?
·         Nini wajibu wa serikali kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu?

Hayo ni miongoni mwa maswali ambayo kama mwana jamii unaweza kujiuliza na kuona ni kwa namna gani unaweza kuwa mwanaharakati wa elimu ya watoto wako na wa jirani yako. Ni kweli tunao wajibu wa kubadilisha namna yetu ya kufikiri kuhusu elimu na maendeleo ya jamii yetu.
Neno mazingira magumu linaweza kukosa maelezo ya moja kwa moja kumuelewesha mtu mpaka akaelewa, ila kwa faida ya hoja yangu ya msingi itoshe kusema ni hali ya umaskini wa kipato uliokithiri unaomkabili mtoto na familia inayomlea. Kwa hapa nchini kwetu Tanzania zipo kaya ambazo zinaishi kwa pato la chini ya dola moja ya Kimarekani. Ni kawaida katika Nyanja ya kiuchumi kufanya ulinganifu wa hivyo kuhusiana na kipato cha kaya moja na nyingine.

Watoto wanaoishi katika mazingira magumu wana changamoto kubwa katika suala la upatikanaji wa elimu, wanakosa mambo mengi ya msingi ikiwemo motisha ya wao kupenda maisha ya kujifunza kama ilivyo kwa watoto wengine wa rika lao. Wanakosa vifaa muhimu vya kuwawezesha kumudu changamoto za kielimu mfano; sare za shule, viatu, madaftari, kalamu, vile vile kwa wanaokaa mbali na shule suala la usafiri na upatikanaji wa chakula.

Mwanafalsafa wa kigiriki anayeheshimika sana duniani katika masuala ya kielimu alipata kunena mtu aliye na njaa hawezi kumudu kufanya tafakari nzuri. Kwahiyo ni wazi inahitaji mtu aweze kuwa na amani ya nafsi na mwili wake kwa ujumla ili aweze kumudu suala zima la kushiriki katika kujifunza. Unapozungumza kuhusu mtoto anayeishi katika mazingira magumu huwa anapitia maangaiko makubwa sana ya kimaisha ambayo ni ngumu sana kumpa motisha ya kupenda kufuatilia masomo.

Mazingira magumu ni magumu hasa, kwani mtoto anapotoka shuleni baada ya kazi kubwa ya kujifunza aliyoifanya akiwa shuleni, arudipo nyumbani angependa akute mazingira mazuri yaliyo rafiki. Ikiwemo wazazi ama walezi wenye furaha na amani, akute chakula cha kumuwezesha kurudisha nguvu yake aliyoipoteza shuleni. Lakini mazingira hayo ni nadra kwa watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu hilo kwa kiasi kikubwa linachangia watoto hao kuchukua uamuzi wa kuacha shule ili waweze kupata muda wa kujitafutia pesa za kujikimu ikiwemo na kulea familia zao pia.

Katika jamii zetu wapo watoto wadogo wanao wajibika kutunza familia zao, bila kujali huo umri wao mdogo. Kaya maskini kwa hakika zina msukumo mbaya kwa maisha ya watoto wao. Wapo watoto wanaoingia katika ajira zisizo rasmi ikiwemo wizi na biashara ya ukahaba ili waweze kupata pesa za kusaidia familia zao.

Ni jambo linalohitaji mkakati mzuri wa kimaendeleo kwa jamii yetu kuona umuhimu na namna nzuri ya kuweza kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili kuepushia taifa letu janga kubwa linaloweza kutokea kwa kuwa na kundi kubwa la vijana lisilo na elimu stahiki. Ingawa si nia ya hoja yangu lakini si vibaya nikisema tukio lililotokea la vijana wanaojiita “Panya Road” ni ishara ya jamii iliyokithiri katika hali duni ya kimaisha. Kwa kuwa kundi kubwa la vijana waliostahili kuwa shuleni na wengine vyuoni ndio hao wanaoshiriki katika vitendo vya uhalifu.

Bila juhudi ya makusudi kukabiliana na suala hilo la kuwapatia watoto na vijana wetu elimu, basi tutarajie mambo kama hayo yakitendeka mara kwa mara. Hivyo kwa namna moja ama nyingine hata waliopata nafasi ya kusoma hawatakuwa tena na amani ya maisha yao kwa kuwa wale wasiosoma watahitaji kugawana nao pato lao kwa kutumia nguvu zao kwa kuwakaba na hata kuwaua.


Nb: Mada hii itakuwa na mwendelezo wake kwa kuendelea kujadili suala la elimu kwa mapana yake, ili wazazi na wadau wa elimu kupata nuru ya kufanya maamuzi sahi

Saturday, February 14, 2015

How to Survive a Boring Lecture.




It happens all the time: to everyone , we all have experienced boring teachers, subjects that are compulsory and not  interesting at all, you're in the middle of a class that is so boring,  Whether the teacher or the subject itself or both are boring, you get headache and sleepy It’s true.  Some lectures could be more effective at putting you to sleep than attentive.  Nevertheless, attending lectures remains a key ingredient for performing well in college.But falling asleep during a lecture isn't going to win you any points with your professor, Try the following tips, which will help you stay awake during those 45 or 1 hour of lecture hell.

Scare yourself straight. "If I don't pay attention to this lesson and remember every single sentence the teacher says I'll never get into college. If I don't get into college, I'm never going to earn my degree. I'll end up 35 years old, still living with my parents and no hopes of getting my own house and family. No one will respect or dare depend on me for advice or anything. Say those words to yourself, scare yourself that way and you will pay attention.

 Use the lecture as an inspiration. "Sitting there listening to the teacher  ramble endlessly about the benefits of chlorophyll really makes you realize that you've been taking your free time for granted. Perhaps you think chlorophyll is not in your life not in your interests and and hence the knowledge of it  will not benefit you in your life, but let me tell you that to every lessons there is a test to test the achievement of  it. That will help you try to pay attention and remember the lesson. Its easier to put up a boring lecture than getting over that pain of failing your exams that you have been working for almost all the time of your life.

 Even A students get bored by lectures.  What is the difference between the A student and the C student?  Their approach to the lecture.  Don’t let “boring” become an excuse for not showing up to class.  Dive right in, sit near the front ,chew gum, and simply face the fact that you will be less than entertained for a couple of hours.  Get in the mental game and you will survive. OMG, this class is so boring!  How are you going to get through it?


  One of my friends from graduate school took impeccable notes, and before exams everyone lined up to study with him.  When I asked him his secret his response surprised me: “I’m bored in class, so I write everything down.” That is an A student approach to the problem!  Instead of avoiding lecture he planted himself close to the front of the room and made it a bit of a game to literally write down word for word what the professor said.  Give it a try.

    Absolutely read the material before class.  If you are unfamiliar with the course material then it will only magnify the boredom.  Not reading would be like signing up for a book club, going to the gathering but never bothering to open the book.  . How boring!  Be sure to prepare and stay in the loop.

  When you are reading the material create possible questions to ask in class (if the professor takes questions).  Participating in class speeds up time for you.  And, you never know, your question could prompt others to speak up and the class could take an intriguing turn.  Dare I suggest, you might enjoy the class then.

    Do not take out your phone to answer , chat or read emails.  Again, this will make the boredom worse.  You are essentially running away from the problem by turning to the cell phone rather than confronting the issue head on.  This is a C student response.  Moreover, it is a bad habit.  After college you might find yourself in other boring situations like work meetings.  It is not a good (or beneficial) idea to tune out and gravitate to your phone while others are talking.  Indeed, there will be times when your good friends bore you!  Would you take out your phone while they talk?  Of course not.  For class time, strengthen your concentration abilities and keep the phone in your bag.

   This last point is a bit painful but it must be made, namely, are you making an effort in the class?  Finding something interesting, like recognizing beauty, takes time and thought.   Often, interest is the result of devoting energy to appreciation of said subject (or object).  When you learn more you will discover more things to be interesting.  The boring lecture just might-maybe-possibly 

-I’m-sorry-to-point-it-out, be indicative of your disposition rather than the professor’s.

Overall, keep the end goal in mind: to do well.  We’ve all been through a boring lecture.  You will survive!  Remember, it is your grade on the line, so don’t shy away from the class even if you need to muster all of your brain power to stay alert.

  Good luck!




Friday, February 13, 2015

Elimu Yetu: Elimu Yetu: JE MZAZI UNAYAJUA MAJUKUMU YAKO KWENYE...

Elimu Yetu: Elimu Yetu: JE MZAZI UNAYAJUA MAJUKUMU YAKO KWENYE...: Elimu Yetu: JE MZAZI UNAYAJUA MAJUKUMU YAKO KWENYE MAENDELEO Y... : JE MZAZI UNAYAJUA MAJUKUMU YAKO KWENYE MAENDELEO YA ELIMU ? Na Makir...

Friday, February 6, 2015

Elimu Yetu: JE MZAZI UNAYAJUA MAJUKUMU YAKO KWENYE MAENDELEO Y...

Elimu Yetu: JE MZAZI UNAYAJUA MAJUKUMU YAKO KWENYE MAENDELEO Y...: JE MZAZI UNAYAJUA MAJUKUMU YAKO KWENYE MAENDELEO YA ELIMU ? Na Makirita Amani Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na anguko kubwa s...

JE MZAZI UNAYAJUA MAJUKUMU YAKO KWENYE MAENDELEO YA ELIMU ?



JE MZAZI UNAYAJUA MAJUKUMU YAKO KWENYE MAENDELEO YA ELIMU ?

Na Makirita Amani

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na anguko kubwa sana kwenye maendeleo ya elimu. Wanafunzi wengi sana wamekuwa wakifeli katika mitihani yao hasa ya kidato cha nne. Katika kufeli huku lawama nyingi sana zimetolewa kwa watu wanaohusika na kuporomoka huku kwa elimu.
Tumeona kila mtu akilaumu serikali kwa kutoweka kipaumbele kwenye maendeleo ya elimu. Serikali imelaumiwa kwa kujenga shule nyingi ambazo hazina walimu, vitabu au maabara. Na pia serikali imelaumiwa kwa kutojali maslahi ya walimu na hivyo walimu kufanya kazi kwenye mazingira magumu na hivyo kuchangia kushuka kwa elimu.
Tumeona pia walimu wakilaumiwa sana kwenye kushuka huku kwa elimu. Walimu wanalaumiwa kwa kutozingatia majukumu yao na hivyo wanafunzi kukosa masomo. Na pia walimu wanalaumiwa kwa kuwa na mgomo baridi ambao unapelekea wanafunzi kukosa usimamizi mzuri shuleni na hivyo kupunguza ufaulu.
Hayo ndio makundi mawili ambayo yamelaumiwa sana kwenye kushuka kwa elimu yetu. Je hawa tu ndio wanaostahili lawama? Je upi ni mchango wa wazazi katika kukua na kuporomoka kwa elimu yetu? Ukweli ni kwamba wazazi wana nafasi kubwa sana katika kukua au kuporomoka kwa elimu. Kwa wanafunzi 
wanaosoma shule za kutwa, wanatumia muda mwingi nyumbani kuliko wanaotumia shuleni. Hii ina maana kwamba kama wazazi wangekuwa makini na maendeleo ya watoto wao shuleni wangekuwa watu wa kwanza kufuatilia kama watoto hawafanyi vizuri. Lakini hiki sio kinachotokea. Wazazi wamesahau kabisa majukumu yao na kuona walimu ndio wenye majukumu yote kuhusiana na elimu.
Ugumu wa maisha umewafanya wazazi kufanya kazi kwa muda mrefu na hivyo kukosa muda wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni. Wazazi wanaamini kwamba kwa kulipa ada shuleni ndio wamekamilisha wajibu wao kwenye elimu. Hii sio sahihi kabisa.

Yafuatayo ni majukumu ya kila mzazi katika maendeleo ya elimu ya mtoto 

1.       Mzazi anatakiwa kujua vipaji vya mtoto wake. Mzazi ndio anakuwa karibu sana na mtoto hata kabla hajaenda shuleni. Kwa kuwa nae karibu anaweza kuona ni vitu gani mtoto anapendelea na hivyo kufanya. Kwa kujua vipaji vya mtoto kutamfanya mzazi aweze kuashauriana na walimu jinsi ya kuweza kuendeleza vipaji vya mtoto wake.

2.       Mzazi anatakiwa kujua maendeleo ya kila siku ya mtoto wake shuleni. Mzazi usisubiri ripoti ya nusu mwaka au ya mwaka kujua mtoto wako amekuwa wa ngapi darasani. Unatakiwa kufuatilia maendeleo ya mtoto wako kila siku. Jua ni kazi gani amepewa za kufanya nyumbani na hakikisha amezifanya kwa usahihi. Pia mzazi anatakiwa kujua maendeleo ya mtoto wake kinidhamu, maana bila nidhamu mtoto hawezi kufaulu vizuri.

3.       Mzazi anatakiwa kujua changamoto ambazo mtoto anazipitia shuleni. Inawezekana mtoto anaonewa na wanafunzi wenzake ila anaogopa kumwambia mwalimu kwa sababu ataonewa zaidi. Wewe kama mzazi ukiwa na urafiki na mtoto wako itakuwa rahisi kuona pale ambapo anapitia changamoto mbalimbali. Kwa kujua hivyo unaweza kuangalia njia nzuri inayoweza kumsaidia mtoto wako ili aweze kuwa na mazingira mazuri shuleni.

4.       Mazazi anatakiwa kumjengea mtoto wake mapenzi mazuri na elimu ili mtoto awe na mtizamo mzuri kuhusu elimu. Mzazi anatakiwa amweleze mtoto kwa nini ni muhimu kwake yeye kusoma na kufaulu vizuri. Pia ampe moyo pale ambapo anashindwa na kumhamasisha kuweka juhudi zaidi kwenye masomo yake.
5.       Mzazi anatakiwa kumfundisha mtoto mambo ambayo hapati nafasi ya kufundishwa shuleni. Sio mambo yote muhimu kwenye maisha mtoto anafundishwa shuleni, kama mzazi atapata nafasi ya kukaa na mtoto wake anaweza kumfundisha mambo ya ziada ambayo yatamsaidia shuleni na hata kwenye maisha.

Mzazi una jukumu la kwanza kabisa katika maendeleo ya mtoto wako kielimu. Acha kukwepa majukumu yako kwa kufikiri kwamba kulipa ada kubwa kunatosha wewe kumsaidia mtoto wako kwenye elimu. Maendeleo ya elimu yanahitaji ushirikiano mkubwa sana kati ya mwanafunzi, mzazi, mwalimu na serikali. Kila mmoja acheze nafasi yake ili tuweze kuendeleza elimu yetu