Sunday, March 8, 2015

Kuelekea siku ya wanawake duniani, Tazama wanawake hawa na harakati zao katika kuboresha kiwango cha elimu.



       Kuelekea siku  ya wanawake duniani, Ningependa kuthamini michango ya baadhi ya wanawake duniani. Wanawake wengi wamesisitiza kuhusu  umuhimu wa elimu kwa wanawake na  jamii kwa nguvu zao zote hapa Tanzania na  duniani kote.
Leo ningependa kutoa shukrani zangu za dhati sana kwa wanawake jasiri na walioamua kuwa mfano bora kwa wanawake wengine na jamii kwa ujumla kwa kufanya mikutano na kuanzisha mashirika mbalimbali ambayo yamekuwa chachu katika maendeleo ya elimu Tanzania na duniani kote.
 Orodha inaanza na hawa wafuatao:

MICHELE OBAMA

Huyu ni mke wa Rais wa Marekani Barrack Obama. Mwanamke huyu alisema "Education is the most important civil right issue" elimu ni haki muhimu zaidi katika haki za kiraia za mwanadamu. Pia alianzisha kampeni inaitwa "Let Girls Learn " katika nchi za Asia ambapo alienda kufanya kampeni za kuhamasisha elimu kwa wasichana .

MAMA SALMA KIKWETE

Mama Salma kikwete , Mke wa Rais wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete. Alianzisha 'WANAWAKE NA MAENDELEO' ( WAMA ) shirika ambalo limekuwa linatoa kipaumbele kwa wasichana kupata elimu. WAMA ilianzisha shule ya WAMA Sharaf Secondary School mwaka 2010 huko Lindi ambapo ilisaidia wanafunzi 400 kwa wakati huo mwaka 2014 iliendeleza masomo ya elimu ya juuyaani kidato cha tano na cha sita.

MAMA MAAJAR

HASSAN MAAJAR TRUST ilianzishwa  ili kuboresha mazingira ya elimu na kujifunzia kwa kuchangia madawati yaani " mobilizing funds for school furnitures"  Ilianzisha kampeni ya "desk for every child" na kufanikiwa kuwainua watoto wengi na kuwaweka katika madawati nchini Tanzania.

FLAVIAN MATATA


Dada yetu huyu ni mwanamitindo lakini pia ni mwanzilishi wa FLAVIANA MATATA FOUNDATION ambayo inafadhili wasichana katika elimu na kugawa vifaa vya shule kwa wanafunzi waliopo katika mazingira magumu kwa kujifunzia na kufundishia.


JUDITH WAMBURA "lady jay dee"


Mwanamuziki huyu mashuhurri na mfano wa kuigwa kwa kushiriki kwake katika elimu kwa kuchangia madawati ya wanafunzi katika shule ya bungoyi iliyopo shinyanga na kuahidi awamu nyingine atatoa tena january mwaka huu kwa ajili ya madawati na ujenzi wa vyoo katika shule hiyo.

TGNP (TANZANIA GENDER NETWORK PROGRAM ) ilianzishwa 1993 na kusajiliwa mwaka 2012 kwa dhumuni la kusimamia usawa katika haki za wanawake, ( GENDER EQUALITY )



Shirika hili lisilo la kiserikali linasaidia wanawake wengi tanzania kwa kampeni mbalimbali za kupunguza na kutokomeza unyanyasaji wa wanawake hapa Tanzania kwa mikutano mbalimbali na machapisho hata katika mitandao ya kijamii.


 REBECA GYUMI
Kama wewe ni mpenzi wa kipindi cha FEMA utajua Rebeca ni nani. Ni mwanamke jasiri na mtaalamu wa mambo ya jinsia na elimu. Amekuwa mtangazaji wa kipindi hiki tangu nipo mdogo sana na mpaka leo namuona  anafanya kazi ile ile, yaani hapo utaelewa kwamba ni mapenzi yake kufanya kazi hiyo ya kuelimisha vijana kuhusu mambo mbalimbali ya elimu na ujinsia.



TAWLA
TANZANIA WOMEN LAWYERS ASSOCIATION , chama cha wanawake wanasheria Tanzania ambacho kinatoa msaada wa kisheria na elimu ya sheria na haki za wanawake . Wanawake wengi waligubikwa na umasikini kwa sababu ya talaka miaka ya nyuma hapa nchini lakini leo hawa wanawake shujaa wametengeza mahali pa kukimbilia kama kituo cha msaada kwao.


     Hawa ni baadhi ya wanawake ambao juhudi zao katika kujenga jamii zinaonekana kwa macho na kwa vitendo , na najua wapo watu wengi wanaona wanachofanya na wanafurahishwa na juhudi zao.  Pia naomba jamii kwa ujumla ijitokeze kushiriki katika kampeni mbalimbali wanazofanya na kuwaunga mkono. Wanawake wote kwa ujumla wanashiriki katika kujenga jamii, wazazi, walezi , wanahabari wanawake pamoja a wanasheria, NA katika siku hii  ni muhimu kutambua michango ya wanawake katika jamii na kuunga mkono harakati zao,











0 comments:

Post a Comment