Tuesday, October 7, 2014

Watoto pia wanaweza, kazi zao zinapendeza .

       Mpe nafasi mtoto/mwanafunzi wako ya kumuwezesha kuwa mbunifu na kuendeleza kipaji chake. Hii itamsaidia kuongeza uwezo wake wakufikiria, wa kujiamini, pia uwezo wa kujiajiri katika maisha yake ya baadaye.

Vilevile kuwapa watoto nafasi ya kuunyesha ubunifu wao na vipaji vyao itawapa uwezo mkuubwa wa kukumbuka kwakuwa vitu vyote ametumia uwezo wake mwenyewe. Nilienda mikocheni shule ya msingi ambapo kulikua na tamasha dogo linaitwa TAMASHA LA VITABU VYA WATOTO DAR ES SALAAM walishirikiana na NAFASI ARTS SPACE ambapo watoto walichora, waliimba , na kusimuliana hadithi. Pia kulikuwa na vitabu maalum kwa ajili ya watoto.







Mtoto akionyesha picha aliyochora.
 Mtoto akionyesha picha aliyochora.
 Vitabu mbalimbali pia vilikuwepo. kwa bei rahisi sana.









                                                                                              Ilikuwa ni siku nzuri na tamasha lilipendeza sana. Bila shaka siku nyingine nitahudhuria.

0 comments:

Post a Comment