Walimu ni kundi muhimu katika jamii ambalo huchangia sana katika malezi ya watoto kimawazo, kiakili na kiuelewa.
Hapa Tanzania mwalimu anatambulika kama mtu aliyefuzu mafunzo ya ualimu na kutunukiwa cheti. lakini je cheti pekee kinatosha kuonyesha mwalimu bora?. Mwalimu ni muwezeshaji na muongozaji wa mawazo ya mwanafunzi, kuyakuza na kuyastawiisha pamoja na kuuboresha ubunifu wa mwanafunzi.
Mwalimu bora ni yupi?. Mwalimu bora ni yule mwenye mbinu mbalimbali za kuhakikisha mwanafunzi anabaki darasani kimawazo na kiakili kivitendo zaidi. Elimu si madarasa, madawati na ufundishaji tu bali ni uwezo wa motto kuelewa anachojifunza.
Huyu ndiye mwalimu anatayekomboa jamii.
Thursday, August 21, 2014
Je, Walimu wetu wameandaliwa kuikomboa jamii?
11:32 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment